Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni ametoa
siku tatu kwa wachezaji raia wa Ivory Coast wanaofanya majaribio pamoja na
kikosi chake kuonyesha wanastahili kubaki au la.
Ingawa vyombo vingi vya habari vimeripoti
wanatokea nchini Nigeria, Kibadeni alisema wamemuambia kwao ni Ivory Coast
nchini anayetokea mshambuliaji nyota Didier Drogba.
“Lazima mambo yaende haraka kidogo, siku tatu
ni kwa ajili ya kuwaangalia kama wataendelea kubaki hapa nasi kwa ajili ya
majaribio zaidi.
“Kama nitaona hawawezi, basi mara moja
nitawaondoa ili kupunguza watu hapa lakini kuendelea na programu yetu ya
mazoezi na watakaoonekana wana msaada.
“Najua muda utakuwa mchache, lakini mambo
mengi yako mbele yetu na tutakiwa kuyakamilisha, hivyo hatutakuwa na muda
kabisa,” alisema Kibadeni.
Leo ni siku ya tatu akiwa kazini, Kibadeni
ameendelea kufanya mazoezi na wachezaji wachache wa Simba huku asilimia kubwa
wakiwa ni wanaofanya majaribio.
0 COMMENTS:
Post a Comment