Na Saleh Ally
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema winga wake
wa kulia, Simon Msuva wala hatakaa benchi kutokana na winga mwingine, Mrisho
Ngassa kujiunga na timu hiyo.
Kujiunga kwa Ngassa na Yanga, imekuwa ni tafsiri kuwa
Msuva ambaye ni kinda, atapoteza namba na wakati fulani, mashabiki wa Yanga
waliwahi kumshambulia kwa maneno wakimueleza kama Ngassa akijiunga na timu hiyo
utakuwa mwisho wake.
Akizungumza moja kwa moja kutoka jijini Barcelona,
Hispania, Brandts alisema Msuva bado ana nafasi na ataendelea kucheza lakini
Ngassa atapata nafasi iwapo atajituma na kumuonyesha kocha anastahili kucheza.
“Msuva ni mchezaji ambaye amekuwa akijirekebisha kila
siku, si lahisi uanze kumuweka benchi tu. Najua anahitaji kujituma na kuonyesha
anastahili kupata namba, analitambua hilo.
“Lakini hata Ngassa, hana namba katika kikosi cha
kwanza, lazima ajue anatakiwa kuonyesha kuwa anaihitaji nafasi,” alisema
Brandts.
Salehjembe: Sasa wote wanacheza namba saba, itakuwaje?
Brandts: Ngassa anaweza kucheza kushoto, lakini baada
ya muda hata Msuva ataweza kucheza pia.
Salehjembe: Labda kipi unaona Ngassa anatakiwa
kuongeza?
Brandts: Yapo mengi, kama kocha nimeyaona na
niyazungumza naye. Lakini suala la kujituma na kuitafuta namba, si namna
imfuate yeye.
Salehjembe: Unarejea lini Dar?
Brandts: Nitaondoka hapa Barcelona baada ya siku
mbili, narudi nyumbani Uholanzi, mwanzoni mwa mwezi ujao nitakuwa Dar.
Salehjembe: Kuna nini kipya Barcelona?
Brandts: Nilikuja kwa mapumziko na familia yangu.
Salehjembe: Kila la kheri.
Brandts: Nashukuru, kazi njema.
0 COMMENTS:
Post a Comment