Na
Mwandishi Wetu
SIMBA
imeonyesha kweli imepania kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake baada
ya kumnasa kiungo mshambuliaji nyota kutoka Uganda, Moses Oloya.
Simba
imelazimika kujipinda na ‘kuvunja benki’ kwa kutoa zaidi ya Sh milioni 40 ili
kumsajili Oloya ikiwa ni pamoja na kufikia makubaliano na wakala wake aliyejulikana
kama DM Management.
Oloya
ambaye amekuwa akiwagawa mashabiki wa soka Uganda, kwamba yeye na Okwi nani ni
zaidi, amekubali kumwaga wino na kuichezea Simba msimu ujao.
Kila kitu
kati ya Oloya na Simba kimemalizika na mchezaji huyo amekubali kuondoka Xuan
Than Saigon inayoshiriki Ligi Kuu ya Vietnam na kujiunga na Simba.
Simba
imekuwa ikifanya siri kubwa kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo wakiwahofia
watani wao Yanga wanaweza kuvuruga mambo na kumsajili.
“Yanga
ndiyo imekuwa hofu kubwa, maana wakisikia Simba wanamhitaji mchezaji na wenyewe
wanamuona anafaa. Hilo ndiyo limekuwa tatizo kwetu.
“Lakini
Oloya amekubali kusaini, mkataba wake utatumwa huko kwa kuwa Uganda The Cranes
itakuwa huko kucheza mechi ya kirafiki Jumamosi hii.
“Kila kitu
kitamalizikia Libya, labda kama kuna mabadiliko lakini kila kitu kimefikiwa
makubaliano,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Oloya
ambaye ana miaka 20 tu, alijiunga na Xuan Than Saigon, Januari Mosi, 2011 na
amefanikiwa kufunga katika mechi kadhaa za kirafiki ingawa anaonekana kuwa
mzuri katika kupiga mabao.
Urefu wake
ni futi 1.80, ana kasi inayolingana na ile ya Okwi, anapiga mashuti miguu yote,
si mzuri sana wa mipira ya vichwa, ana uwezo wa kupiga mipira iliyokufa.
Ndiye
anaaminika kuwa staa mpya wa Uganda ambayo tayari kaichezea mechi 14, mashabiki
wengi wamekuwa wakiamini ni mkali kuliko Okwi.
Tayari
Oloya amejiunga na kikosi cha Uganda nchini Libya, tayari kwa ajili ya mechi
hiyo ya kirafiki dhidi ya wenyeji.
0 COMMENTS:
Post a Comment