M To The P akiwa na Ngwea...siku chache kabla ya matatizo.. |
M To The P, rafiki wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa naye wakati mauti yanamkuta ni mzima.
Lakini taarifa zinaeleza hali yake bado si nzuri na sasa yuko katika chumba cha watu mahututi (ICU) katika Hospitali ya St Helen Joseph jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Taarifa za uhakika kuhusiana naye tumezipata kutoka kwa daktari aliyejitambulisha kwa jina la Robert na kusema bado hali yake si nzuri.
“Anaendelea kupata matibabu, hali yake kidogo ina unafuu, lakini haijawa vizuri,” alisema.
Kuanzia leo asubuhi kumekuwa na taarifa za kuzagaa kwa kifo cha M To The P ambaye alikuwa na Ngwea hadi mauti yanamkuta.
Bado uchunguzi unaendelea kuhusiana na kifo cha Mangwea na tatizo lililowakuta hadi kusababisha hali hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment