May 29, 2013





Hatimaye Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini wamefanikiwa kuuona mwili wa marehamu Albert Mangwea.

Watanzania hao wameuona mwili huo katika eneo la Hillbrow ambako ulichukuliwa na kupelekwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Mmoja wa Watanzania aitwaye Simon amesema kwa pamoja wameingia katika chumba na kuushuhudia.


“Tumeuona mwili wa Mangwea, roho inauma sana. Tuko hapa na watanzania wengine waliotoka huko. Mmoja anaitwa sijui Kinje, lakini kuna mwandishi mmoja hapa (Millard Ayo).

“Mangwea amefariki na kwa kweli inatia huzuni sana, kila mtu ameonekana kujisikia vibaya.

“Baada ya kutoka katika chumba kile, kila mmoja ameonekana kupooza kama kamwagiwa maji. Inauma sana kwa kweli,” alisema Simon.

Asubuhi hii, mwili wa Mangwea ulitolewa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya St Helen Joseph na kupelekwa eneo hilo la Hillbrow kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Ingawa kumekuwa na taarifa zinazozagaa kwamba majibu ya uchunguzi yametoka, lakini Watanzania hao wamesisitiza bado daktari hajatoa majibu.

“Watanzania bado wako wengi hapa, lakini bado majibu hayajatolewa. Tunaendelea kusubiri na sasa tunaendelea katika kuchagua majeneza.”

Msiba uko Mbezi Beach karibu na Goig jijini Dar es Salaam na familia yake imetangaza kwamba inaendelea kufanya taratibu za kuusafirisha mwili.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic