Kisiga (wa pili kulia msitari wa chini) akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar.. |
Klabu ya Mtibwa Sugar imesema haiwezi kuingia katika mtego wa malumbano na kiungo wake Shabani Kisiga ambaye ameamua kujiondoa.
Kisiga amerejea jijini Dar na kuachana na Mtibwa Sugar kwa madai ya kutibuliwa na benchi la ufundi linaloongozwa na Mecky Maxime.
Lakini mara nyingi, Maxime, beki wa zamani wa timu hiyo amekuwa akikwepa kulizungumzia suala hilo lakini Kisiga amesisitiza, yeye na Mtibwa basi.
“Yule sisi ni wa kwetu mpaka sasa na hatuwezi tukaacha
mambo mengine, tunamwacha tu aseme atakavyotaka halafu na sisi tutamtafuta
ikiwezekana ligi itakapoisha na kuamua juu ya hatma yake na klabu hii,” alisema
Maxime.
Kisiga ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba, amerejea
na katika kiwango kizuri baada ya kuachana na kazi ya udereva taxi na kuamua
kucheza tena soka.
0 COMMENTS:
Post a Comment