Baada ya mzunguko wa muda mrefu, hatimaye kipa wa Yaw
Berko amemalizana na uongozi wa klabu hiyo.
Tayari Berko yuko tayari kuondoka na kuendelea na
maisha yake baada ya Yanga kumlipa haki zake.
Berko raia wa Ghana aliondolewa katika kikosi cha
Yanga kwa madai ya kuwa na maringo hali iliyofanya uongozi wa Yanga uone
hajitoi asilimia mia kwa ajili ya klabu hiyo.
Ikaamua kumpeleka kwa mkopo katika timu ya DC Motema
Pembe ya DR Congo ambako baadaye hawakuelewana akaamua kurejea nchini.
Baada ya kurejea, alikuwa akiishi katika makao makuu
ya klabu hiyo kwa kujificha huku ikionyesha wazi hakutaka kuonekana.
Berko alikataa kuzungumzia suala lake, lakini mmoja wa
viongozi wa Yanga, hakutaka kutajwa mtandaoni alisema Berko ameshalipwa stahiki
zake.
“Ataondoka hivi karibuni, ameshalipwa haki zake na
kuna mambo kidogo tu ya kukamilisha,” alisema.
Salehjembe inaendelea kumsaka Berko ili kujua undani wa
suala hilo na ataondoka lini kuelekea wapi.
0 COMMENTS:
Post a Comment