Taarifa zinaeleza mwili wa Mangwea utafanyiwa
uchunguzi kwa mara nyingine.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hospitali ya St Helen
Joseph ya jijini Johannesburg amesema uamuzi huo umetokana na kutokamilika kwa
mambo kadhaa baada ya uchunguzi wa kwanza.
“Kuna vitu havikukamilika, lakini kuna mambo
tumeona kama si sahihi, hivyo tutachunguza tena,” alisema na alipoulizwa
kuhusiana na walichokiona katika ripoti ya kwanza, akajibu:
“Kawaida ndugu zake ndiyo wanatakiwa kupokea
ripoti, huenda ikatoka Jumatatu. Hivyo watapewa watu wanaohusika.”
Mmoja wa Watanzania anaoishi Afrika Kusini,
amesema wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua kilichomuua Mangwea kwa kuwa
taarifa zimekuwa ni za kutatanisha.
“Kweli kila mtu anataka kujua, tatizo linakuwa ni
moja kwamba mambo yanakwenda kwa siri sana.
“Lakini hata kati yetu huku kuna watu wamekata tama
kwa kuwa haijulikani mambo yanakwenda vipi.
“Lakini kuna wengine wanaendelea kuchanga, mfano
kuna daftari linapita huku Hillbrow na kwingine na watu wanaendelea kuchanga.
“Awali tuliambiwa serikali imechukua jukumu,
lakini baadaye wanasema Clouds ndiyo watafanya mambo yote. Sasa kiasi Fulani tunakuwa
hatuelewi kinachoendelea,” alisema Mtanzania huyo anayeitwa Joseph.
Mwili wa Mangwea bado uko katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya St Helen Joseph.
Taarifa zinaeleza mwili huo utaondoka huko
Jumapili mchana na kuwasili jioni kwa kuwa kwa ndege ni mwendo wa saa tatu na
nusu.
Kuagwa kwake itakuwa Jumatatu kuanzia saa 3
asubuhi na baada ya hapo atasafirishwa kwenda Morogoro kwa mama yake ambako
atapumzishwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment