May 31, 2013


Kapinga akiwa kazini, akimtibu Dhaira wakati alipokuwa daktari..


Madaktari 10 wameomba kazi ya kuwatibu wachezaji wa Simba, nafasi ambayo iko wazi baada ya aliyekuwa akiishikilia, Cosmas Kapinga kupata ajira nyingi.

Kati ya madaktari hao 10, akiwemo mmoja raia wa Kenya wameonyesha nia ya kuipata kazi hiyo ya utabibu ndani ya Simba.

Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha kujitokeza kwa daktari mmoja raia wa Kenya.


Alisema Simba inaendelea na mchakato wa kupata mmoja ambaye atapewa kazi hiyo ya daktari wa Simba.

“Kweli tulifanya mchakato wa kusaka daktari mpya ambapo walijitokeza wengi akiwemo Mkenya aliyekuwa akitaka nafasi hiyo ya Kapinga.

“Tunashukuru tumemuona mmoja ambaye ni mzoefu wa kuwatibu wachezaji na yupo kwenye moja kati ya klabu za ligi kuu, hivyo tupo kwenye mazungumzo naye tukimalizana tu tutamuweka hadharani,” alisema Kamwaga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic