Kama kila kitu kitakwenda vizuri, mwili wa
msanii Albert Mangweha utawasili nchini Jumamosi.
Mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini Afrika
Kusini amesema, mipango inaonekana kwenda vizuri na serikali imekuwa ikitoa
msaada.
“Kama mambo yote yakienda sawa, basi Jumamosi
mwili utawasili Dar es Salaam. Lakini bado tunaendelea na michakato mingine.
“Walituambia mwili utafanyiwa uchunguzi leo,
kesho Alhamisi majibu yote yatafanyika na maandalizi ya kuusafirisha yameishaanza
ingawa Ijumaa tunategemea kila kitu kiwe kimekamilika kabla ya safari ya
kumrudisha nyumbani Mangwea kuwa Jumamosi,” alisema Joseph mkazi wa Hillbrow.
“Kama kutakuwa na mabadiliko tutawaeleza lakini
lazima tuwahi kumsafirisha kwa kuwa sheria za Afrika Kusini zinasema baada ya
siku tatu, maiti inatolewa kweye mochwari ya hospitali ya serikali.
“Baada ya hapo, tutalazimika kumpeleka maiti
katika hospitali ya kulipia mochwari. Hivyo tunajitahidi kufanya mambo mengi
haraka."
Mangwea amefia Afrika Kusini, bado kumekuwa na
utata kuhusiana na kifo chake huku taarifa za kwanza zikieleza kwamba
alizidisha dozi ya dawa za kulevya.
Lakini subira ya ripoti ya daktari ndiyo inaweza
ikaeleza kila kitu kuhusiana na kifo cha msanii huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa
wa ‘kutembea’ juu ya verse za hip hop, ka’Obama.
0 COMMENTS:
Post a Comment