May 29, 2013



Martinez akitokea katika mkutano, leo jioni

Kocha wa Wigan, Roberto Martinez amekutana na Mwenyekiti wa Everton, Bill Kenwright na kufanya mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo.
 
Mwenyekiti Everton baada ya mkutano

Martinez aliyeipa Wigan ubingwa wa Kombe la FA ingawa siku chache baadaye iliteremka daraja alikutana na mwenyekiti huyo katika Hoteli ya Landmark katika ya jiji la London na kufanya mazungumzo hayo.

Nafasi ya kocha mkuu wa Everton iko wazi baada ya, David Moyes aliyekuwa anaishikilia kwa zaidi ya miaka mitano kujiunga na Manchester United.

Moyes amechukua nafasi ya Alex Ferguson ambaye alitua Man United mara ya kwanza mwaka 1986 akitokea Aberdeen ya kwao Scotland. Taarifa zinaeleza, uongozi wa Wigan umetoa ruhusa kwa Martinez kuondoka kama kila kitu kitakwenda vizuri katika mazungumzo hayo.

Bado Martinez na Everton hawajafikia mwafaka, lakini dalili zinaonyesha ndani ya siku chache zijazo, timu hiyo itamtangaza Martinez kuwa kocha mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic