July 6, 2013


BIN SLUM

 Uongozi wa klabu ya Coastal Union umekata mzizi wa fitna baada ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na suala la kipa Juma Kaseja.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Mohammed Bin Slum amesema hawana mpango wa kumsajili kipa huyo aliyeachwa na Simba.


“Tuna heshima kubwa sana na uwezo wa Kaseja, pia mchango wake katika soka ya Tanzania. Lakini hatujawahi hata kuzungumza naye kuhusiana na kumsajili.

“Kumekuwa na tetesi nyingi kwamba anakuja Coastal, lakini hatujafanya hivyo kwa kuwa tayari tuna Shabani Kado, tulisajili kipa mpya na kuna mwingine amepandishwa kutoka timu B.

“Watu wengi wanaamini kwa kuwa tumewasajili Boban na Nyosso, basi kila mchezaji mwenye jina kubwa akiachwa, tunamsajili. Si kweli, kawaida tunaangalia mahitaji yetu,” alisema Bin Slum.

Baada ya Kaseja kumaliza mkataba na Simba na uongozi wa klabu hiyo kusema hautamuongezea, kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kwanba huenda akajiunga na Simba.

Taarifa hizo zimefanya wengi kuamini kama si Yanga na Azam FC, basi nahodha huyo wa timu ya taifa, Taifa Stars atajiunga na Coastal Union.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic