January 26, 2019


Mshambuliaji wa Simba, John Bocco sasa amerejea rasmi na atacheza mechi dhidi ya Al Ahly itakayopigwa Februari 2, mwaka huu nchini Misri.

Bocco aliumia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura na kusababisha akose mechi dhidi ya AS Vital ya DR Congo ambayo Simba ililala mabao 5-0.

Simba imepanga kuwafuata Al Ahly keshokutwa Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo. 

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema hali ya mchezaji huyo inaendelea vema kwa sasa na kuna uwezekano akawa sehemu ya kikosi dhidi ya Al Ahly.

“Mshambuliaji wetu John Bocco anaendelea vizuri na mechi yetu ijayo dhidi ya Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika anaweza kucheza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic