Imeelezwa kuwa wachezaji kadhaa wa klabu ya Simba walikesha klabu siku moja kabla ya mchezo na Bandari FC ambao ulimalizika kwa wageni kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Kupitia Radio EFM, Mwanachama wa Simba, Suleiman Yusuph, amewataja wachezaji watano ambao ni hawa wafuatao
1. Haruna Niyonzima
2. Hassan Dilunga
3. Sergi Wawa
4. Mohammed Ibrahim na
5. Jonas Mkude
Simba imefungwa na Bandari timu amba y o haina kiwango cha kutisha na kushindwa kufika fainali ya Kombe SportPesa ambalo mashabiki wake wengi walitarajia kuona wanalibeba.
Suala la wachezaji hao limehamisha gumzp baada ya mashabiki kuanza kumlaumu Kocha Patrick Aussems kwanini hakuanza na wachezaji kadhaa akiweno Mkude.
Kumekuwa na taarifa baadhi ya wachezaji wa Simba walicheza wakisadikiwa kwamba walikuwa wananuka pombe.
Pamoja na Simba kutangulia kufunga katika mechi hiyo Bandari walisawazisha na kuongeza bao la ushindi.
CHANZO: EFM








AIBU SANA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA KAMBI OMBENI MSAMAHA MMETUANGUSHA SANA SANA KWANINI WACHEZAJI HAWAJITAMBUI?
ReplyDeletehakina lolote hapo
ReplyDeleteOhh vipi walienda wapi??.
ReplyDeleteAu walifata machangu Doa.?
Duu
ReplyDeleteSimba wana kikosi kipana hao wengine walikuwa na jukumu gani?
ReplyDeleteHii ni kazi ya meneja bado kuna sehemu uongozi una lega lega
ReplyDelete