Mechi ya marudiano ya Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na Polisi
Jamii ya Mara iliyokuwa ichezwe Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) imesogezwa mbele
kwa siku moja.
Timu hizo sasa zitacheza Jumapili
(Julai 14 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi. Polisi Jamii
ilishinda bao 1-0 mechi ya kwanza iliyochezwa Julai 6 mwaka huu Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Refa Hans Mabena kutoka Tanga ndiye
atakayechezesha mechi akisaidiwa na E. Mkumbukwa na Hajj Mwalukuta wote kutoka
Tanga. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni Kessy Ngao wa Dar es Salaam.
Mechi kati ya Stand United FC ya
Shinyanga na Kimondo SC ya Mbeya itachezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Mwamuzi atakuwa Daniel Warioba kutoka
Mwanza. Kimondo SC ilishinda mechi ya kwanza bao 1-0.







0 COMMENTS:
Post a Comment