![]() |
| MWINA KADUGUDA NAYE AKIPEWA MKONO... |
Wasanii na wanamichezo mbalimbali walionyesha wenye wako ‘shap’ ili
kufanikiwa angalau kupata mkono salamu kwa kusalimiana na Rais Jakaya Kikwete.
Hali hiyo ilitokea wakati wa Tamasha la Matumaini mwishoni mwa wiki
iliyopita wakati Rais Kikwete akishuka jukwaani kwenye uwanjani kukagua timu za
Wabunge wa Yanga na Simba.
![]() |
| JB AKIMWAGA 'SERA'.. |
Kwa kuwa wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva hawakuwa katika programu
ya kumsalimia Rais Kikwete, ‘fasta’ walitengeneza mstari wao na kumvizia akiwa
njiani kwenda uwanjani.
M To The P, rafiki mkubwa wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ alikuwa
kati ya wasanii wa kwanza wa Bongo Fleva waliomsalimia Rais Kikwete na
kufuatiwa na wengine kama Manyika Peter akiwemo nahodha wao H Baba.
Lakini JB na Dk Cheni waliowaongoza Bongo Movie pia kusalimia na Rais
Kikwete.
Katibu Mkuu za zamani wa Simba pia Fat, Mwina Kaduguga pia alionyesha ni ‘shap’
kinoma, baada ya kufanikiwa kusalimia na rais huku wakizungumza “mawili matatu”.
Karibu kila aliyepata bahati hiyo alionekana ni mwenye furaha kupindukia.











0 COMMENTS:
Post a Comment