July 10, 2013



 
TAMBWE (KATIKATI) YA WAZEE WA MSIMBAZI MARA TU BAADA YA KUTUA DAR USIKU HUU

Pamoja na Yanga kuonyesha nia ya kumnasa, mshambuliaji nyota wa Vital’O ya Burundi, Hamis Tambwe ametua nchini tayari kumalizana na Simba.

Tambwe ametua usiku huu, saa 6 akitokea Bujumbura kupitia Nairobi, Kenya na kusema yuko tayari kujiunga na Simba.

“Nimekuja kuwasikiliza, kwa sasa siwezi kusema maneno mengi sana. Inabidi nikutane nao na kujadili.
 
KIMO CHAKE KAMA SALEH ALLY, ILA NI MKALI WA KUCHEKA NA NYAVU

“Kwa kuwa nimefika hapa ninaamini mambi yatakwenda vizuri,” alisema Tambwe huku akisisitiza kweli Yanga walimfuata wakitaka atue Jangwani.

Baada ya kutua, Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa michuano ya Kagame alipokelewa na wenyeji wake Simba ambao walikuwa makini kuepuka watani wao wa jadi Yanga wasije “kukitia kitumbua mchanga”.

Kwa uangalifu mkubwa waliondokana naye na kuingia katika gari lililokuwa likioendeshwa na Meddy na kuingia katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam.

Imeelezwa Tambwe atakuwa mafichoni hadi Simba watakaporejea jijini Dar kesho na kuanza mazoezi nao.

Mshambuliaji huyo ameisaidia Vital’O kutwaa ubingwa wa Kombe la Kagame lakini pia ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo iliyomalizika Sudan wiki siku chache zilizopita.

Pamoja na hivyo, Tambwe amekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Burundi baada ya kufanikiwa kupachika mabao 18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic