Mshambuliaji mwenye vituko wa Liverpool, Luis Suarez amekata mzizi wa fitna baada ya kurejea katika kikosi cha timu hiyo.
Pamoja na kuwa na taarifa kwamba amekuwa akisisitiza kutaka kuondoka na kujiunga na Real Madrid ya Hispania, Suarez amejiunga na wenzake walioko nchini Australia.
Imeelezwa Kocha Brendan Rodgers atampanga katika mechi ya kirafiki keshokutwa jijini Melbourne.
Kurejea kwa mshambuliaji huyo maana yake kumepunguza kasi ya hisia kwamba huenda atajiunga na Madrid.
Mashabiki wengi wa Liverpool walikuwa kama ataondoka hali ambayo igeyumbisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Katika mazoezi ya leo, Suarez alionyesha ni mwepesi na alikuwa mwenye furaha.
Ukichana na hivyo, mashabiki wengi walionyesha kuvutiwa zaidi na Suarez na hata baada ya kupata taarifa alikuwa katika kikosi hicho walichanganyikiwa zaidi.
Wengi walitaka kumuona na hata baada ya kuiona sura yake, wengi walishangilia kwa nguvu sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment