July 22, 2013



 

Katika msimu mpya wa 2013-14, Simba na Yanga zitakutana kwa mara ya kwanza Oktoba 2, 2013.

Baada ya hapo, TFF imetoa nafasi ya miezi sita kwa timu hizo kabla hazijakutana katika mechi ya mwisho ambayo itakuwa ni ya kufunga ligi.


Katika mechi hiyo itakayochezwa Aprili 27,2014, Simba watakuwa wageni wa Yanga baada ya kuwa wenyeji katika mechi ya mzunguko huo wa kwanza.
Kitu kigumu zaidi kwa timu zote, mechi ya kufunga msimu inawaangukia wao na kuzidisha ugumu.

Kwa kawaida itakuwa hivi, moja ya timu itakuwa inapambana kuwania ubingwa, nyingine kulinda heshima na ugumu utakuwa wa juu zaidi kama timu zote zitakuwa zinawania ubingwa.



Watani hao bado watakuwa katika wakati mgumu katika mechi za ligi hiyo kwa kuwa Coastal Union, Azam FC, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar zitakuwa kati ya timu zinazoongeza presha kubwa kwao.

Katika ratiba hiyo iliyotolewa na TFF, kila upande utakuwa na kazi ya ziada lakini presha inaendelea kubaki katika mechi hizo mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic