AKIONGOZANA NA MANEMBE PAMOJA NA MTU WA KAZI MEDDY |
Beki mpya wa Simba raia wa Burundi, Kaze Gilbert maarufu kama Demunga,
ametua kwa ajili ya kuichezea timu hiyo inayojiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mrundi huyo alitua jana kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam majira ya saa 10:00
jioni kwa ndege ya Precision Air akitokea Burundi.
Beki huyo alipokewa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo
akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Benchi la Ufundi la
Simba, Danny Manembe pamoja na mpiganaji Meddy ambaye pia ni kiongozi wa
Abajalo ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kutua, alichukuliwa na viongozi hao na
kuelekea hotelini kwa ajili ya kupumzika na kufanya mazungumzo ya kumsajili.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Manembe alisema kuwa
beki huyo ndiyo watakayefunga naye usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
“Huyu Mrundi ndiye tunatarajia kufunga naye usajili
kwa wachezaji wa kigeni na wazawa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Tunatarajia
kuingia naye mkataba wakati wowote kuanzia sasa baada ya kufikia muafaka,”
alisema Manembe.
Akizungumza na Championi Ijumaa, beki huyo alisema:
“Simba wameniita kwa ajili ya kufanya mazungumzo kabla ya kusaini, ninaamini
tutafikia muafaka mzuri na nitasaini.
0 COMMENTS:
Post a Comment