August 1, 2013



 
Pelé amesema mshambuliaji mpya wa Barcelona, Neymar atakuwa bora zaidi ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Pele amesema Neymar raia wa Brazil kama yeye anahitaji kuzoea kidogo tu kabla ya kuchukua usukani wa La Liga na baadaye dunia nzima.

Mkali huyo ameendelea kumsifia Neymar bila ya kujali aliwahi kusema hivyo lakini baadaye ikashindikana baada ya Messi kung’ara zaidi.

Neymar amejiunga na Barcelona akitokea Santos ya Brazil na tayari kumekuwa na gumzo kubwa kati yake na Messi nani atafanya vema zaidi.

Lakini Neymar amekuwa akisisitiza kuwa amejiunga na Barcelona kwa ajili ya kumsaidia Messi kuendelea kung’ara, maneno yanayoonekana kuwa ni hadithi tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic