DEMUNGA BAADA YA KUTUA SIMBA |
Uongozi
wa Simba umeamua kufunga safari hadi nchini Burundi kuhakikisha wachezaji wake wawili Kaze Glibert 'Demunga' na Amis Tambwe wanapata Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amesema wameamua kufanya hivyo ili kupata uhakika wa wachezaji hao kuitumikia Simba.
"Tumefuata taratibu zote lakini tunaona wanatufantia uhuni, hawa jamaa (Vital'O) walikuwa wamemaliza mkataba na wachezaji hawa.
"Lakini bado wakalazimisha wapewe fedha, nasi tukaona haina tatizo, kweli tulitoa dola 10,000.
"Sasa ajabu, bado wanaendelea kushikilia uhamisho wao, wachezaji wako tayari na timu. Inabidi kwenda, ingawa sijajua nani atafita huko.
"Inawezekana nikaona mimi au mtu yoyote wa Simba ambaye atalishughulikia suala hili ili wacheze mechi ijayo."
Taarifa zinasema Shirikisho la Soka la Burundi na Vital'O zinataka wachezaji hao wabaki baada ya Burundi kufuzu michuano ya Chan.
"Kweli wanaona kuwakosa ni kosa, walikuwa na mchango mkubwa katika michuano ya Chan na sasa wanataka kufanya hivi, eti wawatoe Simba kwa mkopo badala ya kama sasa ambavyo wameingia mkataba na timu hiyo.
"Inaonekana ni ujanja wa Warundi na shirikisho lao ndilo linaendesha mpango huu ili wacheze Chan huko Afrika Kusini lakini si kitu sahihi," alisema mpasha habari mmoja kutoka nchini Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment