Uongozi
wa Simba umeendelea kupambana na tayari umefinikiwa kuhakikisha
wachezaji wake wengine waliokuwa na matatizo kama Betram Mombeki na Abel
Dhaira wanacheza.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amethibitisha kwamba wachezaji Mombeki na Dhaira wataichezea timu hiyo leo mjini Tabora dhidi ya Rhino.
"Kulikuwa na mambo kadhaa ya kushughulikia, tumefanikiwa na sasa watacheza mechi ya leo. Dhaira kibali anacho," alisema.
Awali Mombeki alikatiwa rufaa na Pamba ya Mwanza lakini Simba imesisitiza kumaliza suala hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment