Beki Shomari
Kapombe, leo anaweka rekodi mpya katika soka Tanzania pale atakapoanza kazi kwa
mara ya kwanza kama mwajiriwa wa AS Cannes ya Ufaransa.
Kapombe
anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza soka la kulipwa nchini Ufaransa, ingawa iko
daraja la nne kwa sasa, lakini ni timu yenye historia kubwa katika soka nchini
humo.
AS Cannes
ni timu maarufu kwa ajili ya kukuza na kuuza wachezaji barani Ulaya na kati ya
iliyowakuza ni viungo nyota duniani, Zinedine Zidane na Patrick Vieira
waliowahi kutamba katika ligi kubwa kama England, Ufaransa, Italia na Hispania.
Kapombe
amesafiri jana kutoka Uholanzi kwenda Ufaransa kwenda kujiunga na timu yake
hiyo mpya, ikiwa ni siku moja baada ya klabu yake ya Simba kukubali kumuachia.
Simba
imeamua kumuonyesha uungwana Kapombe lakini imewekeza kibiashara kwa kuwa kama
atauzwa, itaingiza fedha kutokana na mauzo hayo.
Wakala
wake, Denis Kadito, jana alithibitisha kuwa Kapombe ametua katika kikosi cha
timu hiyo nchini Ufaransa na leo ataanza mazoezi.
“Kweli
kesho (leo) ndiyo ataanza mazoezi na timu yake mpya, hivyo ni kitu kizuri
ambacho tunapaswa kuamini siku moja kitazaa matunda.
“Mimi
nawashukuru Simba kwa kuwa waelewa katika suala hili ambalo lilihitaji utulivu
sana. Sasa kazi ni kwake Kapombe kupambana kupata namba na baadaye timu
nyingine nzuri zaidi,” alisema Kadito.
Kapombe
alifuzu majaribio katika timu hiyo wakati zaidi ya wachezaji 10 kutoka Ulaya
wenye asili Afrika Magharibi walikuwa wanawania kusajiliwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment