Pamoja na
kuendeleza mgomo wa kutotaka kucheza soka katika kikosi cha Etoile du Sahel ya
Tunisia, bahati nyingine imemuangukia kiungo wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi.
Okwi raia
wa Uganda ameitwa kukipiga katika kikosi cha timu ya Ajax Cape Town ambayo
imesisitiza inataka ianze kufanya naye kazi.
Habari za
uhakika kutoka jijini Kampala zinaeleza, Ajax Cape Town, imemueleza wakala wa
Okwi kwamba inataka kuimarisha kikosi chake kwa kumsajili Okwi.
“Wamesema
wanamtaka aende kucheza katika kikosi chao, wanajua kuhusiana naye na wanasema
walianza kumfuatilia baada ya Kaizer Chiefs kumtaka lakini mwisho
ikashindikana,” kilieleza chanzo cha uhakika.
“Tatizo
moja, hapa lazima Simba walipwe fedha zao dola 300,000, hivyo kunakuwa na
mzunguko. Lakini ambacho tumefanya tumewataka Ajax wazungumze na uongozi wa
Etoile Du Sahel kuhusiana na mchezaji.
“Lakini
wakati huo huo, tumewaambia hali halisi kwamba kuna ishu hii ya malipo, kuwa
Etoile wanadaiwa na Simba, ingawa wao Ajax haiwahusu, lakini vizuri tu wajue.”
Okwi bado
yuko nchini Uganda anaendeleza mgomo wake wa kutorejea Tunisia kwa madai
hawajamlipa mshahara wake tokea Februari, mwaka huu.
Hivi
karibuni, uongozi wa Etoile pamoja na kusisitiza hadi Septemba watakuwa
wamelipa deni hilo, lakini walijaribu kuwashawishi Simba wamchukue na kumuuza,
kitu ambacho Msimbazi walikikataa.
0 COMMENTS:
Post a Comment