August 17, 2013


Dk ya kwanza: mpira unaanza na Yanga wanaonekana kupania zaidi kwa kupeleka shambulizi
Dk 2, BAOOO, Yanga wanafunga kupitia Salum Telela aliyeunganisha pasi ya Abdul Juma.
Dk 5 Azam FC wanazinduka na kufanya mashambulizi mfululizo. Hata hivyo Yanga wanaokoa.

Dk 7, kipa Aishi Manula analazimika kufanya kazi ya ziada kumthibiti Msuva ambaye alikuwa analekea kufunga.
Dk 10, Yanga wanafanya shambulizi jingine, lakini David Mwantika anakuwa makini.
Dk 12, BArthez anafanya kazi yaziada kuokoa shuti la Bocco, anagongana na Yondani.
Dk 13, Yondani anatolewa nje na nafasi yake inachukuliwa na Mbuyu Twite.



Dk 20, Azam wanafanya shambulizi kali, Khamis Mcha akiwa amebaki peke yake na nyavu anashindwa kuusukuma mpira wavuni. Barthez anaumia na sasa anatibiwa.
Dk 22, baada ya kutibiwa, Barthez anasema ameshindwa kuendelea, nafasi yake inachukuliwa na Deogratius Munish ‘Dida’.
Dk 30, shuti kali la Tchetche linagonga mwamba na kutoka nje, inaonekana beki ya Yanga kama haijatulia.
Dk 32 Tchetche anapiga shuti tena baada ya kupokea pasi ya Sure Boy lakini Dida analidaka kiulaini.

Dk 34, Juma abdul anaouga shuti kali linatoka sentimeta chache juu ya lango la Azam.
Dk 36, Manula anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Juma Abdul, mabeki wake wanajigonga na mpira unabaki hauna mwenyewe lakini washambuliaji wa Yanga wanashindwa kuwa shap.

Dk 38, Azam wanafanya shambulizi kali, Twite na Dida wanafanya kazi ya ziada kundosha hatari.
Dk 4 za nyongeza, mwamuzi Oden Mbaga analalamikiwa na wachezaji wa Yanga kwa maamuzi yake
DK 45, Tegete anapiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Kavumbagu lakini inatoka nje sentimeta chache

HALF TIME:
Dk 47, Azam wanaanza na kushambulia lakini Dida anada kifundi krosi safi ya Nyoni.

Dk 49 tayari Azam FC wamefika langoni mwa Yanga mara nne, lakini Yanga hawajafika hata mara moja.
Dk 50, Bocco anaukosa mpira akiwa hatua tatu kutoka kwenye lango la Yanga
Dk 52, mwamuzi Mbaga anatoa kadi ya njano kwa David Mwantika baada ya kuwaangusha Tegete na Msuva.
Dk 54, Manula anadaka shuti kali la faulo la Cannavaro.
Dk 57, Manula tena analazimika kutoka langoni na kumuwahi Kavumbagu
Dk  58 anashindwa kufunga wakati mashabiki wa Yanga wakiwa wameishaamba vitini.
Dk 60, Azam FC wanamtoa Nyoni kaingia Jockins Atudo (Mkenya).
Dk 62, Azam wanamtoa Kipre Balou anaingia Ibrahim Mwaipopo.
Dk 64, Azam wanatapata kona baada ya Twite kufanya kazi ya ziada kuondoa mpira miguuni mwa Mwaipopo wakati akiajiandaa kupiga.
Dk 67, Telela nusura aipatia Yanga bao, lakini Azam wanafanya shambulizi la Nguvu, Bocco naye anajosa bao la wazi
Dk 68, Yanga wanamtoa Tegete na nafasi yake inachukuliwa na Hussein Javu. 
Dk 69, Twite analala na kuokoa lakini anamkuta Bocco ambaye analazimika kutibiwa na baadaye kutolewa, lakini anaomba kurudi.
Dk 74, Azam wanamtoa Bocco anaingia Gaudence Mwaikimba.
Dk 77, Azam FC wanalazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa shambulizi la Yanga baada ya Telela kubaki yeye na kipa.
Dk 78, kichwa cha Kavumbagu kinapita pembeni kidogo mwa lango la Azam FC.
Dk 80, timu zinaonekana kucheza katikati zaidi, hakuna wanaopeleka mashabulizi makali
Dk 85, Twite analazimika kutibiwa nje ya uwanja baada ya kugongwa usoni na Mwaikimba.
Dk 86 Azam Fc wanafanya shambulizi kali, lakini kichwa cha Mwaikimba kinashindwa kulenga lango.
Dk 90, Twite anarejea uwanjani na mashabiki Yanga wanashangilia kwa nguvu, lakini wakati huo Dida anaendelea kutibiwa.
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
MPIRA UMEKWISHAAA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic