Simba imelazimishwa sara ya bao 1-1
dhidi Kombaini ya Jeshi la Polisi katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar.
Vijana wa Abdallah Kibadeni walikuwa wa
kwanza kupata bao lililofungwa katika dakika ya 16 na Betram Mombeki.
Mombeki aliyesajiliwa msimu huu na
Simba, alifunga bao hilo kwa shuti kali.
Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na
mashabiki wa Simba walikuwa wakishangilia kwa nguvu kuonyesha wana hamu ya
kukiona kikosi chao kinaongeza mabao zaidi.
Kipindi cha pili, Simba ilikianza kwa
kasi na kusukuma mashambulizi mengi mfululizo lakini Mombeki, Sino na Ramadhani
Chombo ‘Redondo’ walipoteza nafasi.
Mkongwe Bantu Admini, alitoa basi safi
kwa Nicholas Kabipe ambaye aliandika bao zuri katika dakika ya 58.
Admini tena alitoa pasi nzuri kwa
Kabipe katika dakika ya 66, lakini akashindwa kuwa makini kupachika mpira
wavuni.
SIMBA:
Andrew Ntalla, Nassor Masoud
;Chollo’, Issa Rashi ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Rahim Juma, Jonas Mkude, Said
Ndemla, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Sino Augustino na Ramadhani Chombo
‘Redondo’.
POLISI:
Kondo Salum, Eliasa Maftah, Simon
Fanuel, Yahya Khatib, Salmin Kiss, Salum Nahoda, Magige Machango, Andrew
Bundala, Mokili Rambo, Bantu Admini na Nicholas Kabipe.
0 COMMENTS:
Post a Comment