Blog hii leo imeweka rekodi kuwa ya
kwanza nchini Tanzania kuripoti Live mechi ya Kombe la Ujerumani maarufu kama
Germany DFB Polka, mechi iliyomalizika hivi punde.
Hili ni kama Kombe la FA kwa England na
ilikuwa kati ya timu ya daraja la tano ya Bahlinger SC dhidi ya wageni wao
Bochum.
Bochum ambao wanacheza Ligi Daraja la
Pili Ujerumani au Bundesliga 2, wameibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Hadi Mapumziko, Bochum walikuwa
wanaongoza kwa mabao mawili yote yakiwa yamefungwa kwa ustadi mkubwa na Piotr
Cwielong katika dakika ya 18 na 31.
Kipindi cha pili, wenyeji walionekana
wamepania kuwainua mashabiki wao waliojitokeza kwa wingi uwanjani.
Lakini bado wakashindwa kuhimiliki
mikiki ya Bochum baada ya kufungwa bao la tatu katika dakika ya 63, safari hii
akiwa ni Danny Latza.
Latza aliuwahi mpira wa juu na
kuuparaza kwa kichwa ukawapita mabeki pamoja na kipa na kuandika bao la tatu.
Wenyeji Behlinga walionekana wamepania
kutotaka kuwaangusha watu wao baada ya kufanikiwa bao la kufutia machozi
lililofungwa na Goppert katika dakika ya 90.
Hali ya Uwanja wa Kaiserstuhl ilikuwa
nzuri, watu kibao walijitokeza na shangwe zilikuwa za kutosha lakini hata hivyo
timu yao ikang’olewa.
Mwishoni ilikuwa raha zaidi, kwani
pamoja na kufungwa, wachezaji walizunguka uwanja mzima wakiwapigia makofi
mashabiki kuonyesha wanashukuru nao walijibu mapigo namna hiyo kuonyesha walikuwa
pamoja nao.
DAKTARI MWANAMAMA ALIKUWA KIVUTIO SANA... |
HAPA NIPO NA MAJEMBE YANGU, SHEVA, SEKULE, CARLOS, JAPHETERRY NA RAJAB.. |
0 COMMENTS:
Post a Comment