August 2, 2013

MABUSELA...

Taa ya hatari imewaka kwa beki Vincent Matsobane Mabusela anayefanya majaribio katika kikosi cha Simba.

Mabusela raia wa Afrika Kusini yuko na kikosi cha Simba akiendelea na majaribio.
Hata hivyo huenda akarejea katika timu yake ya Black Leopard ya Afrika Kusini kam Simba itamsaini Kaze Gilbert ‘Demunga’ ambaye tayari yuko nchini.
MABUSELA (WA PILI KUSHOTO) AKIWA MAZOEZINI NA SIMBA.
Demunga ni beki mwenye uwezo zaidi kwa uwa ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Burundi.
Huenda akasaini leo au kesho na hiyo ndiyo itakuwa safari ya Mabusela ambaye bado hajaliridhisha sana benchi la ufundi la Simba.

Beki huyo amecheza mechi moja akiwa na Simba, lakini akaonyesha uwezo wa kiwango cha kati na pili Simba walikuwa na hofu kutokana na umbo lake.

Tayari Simba imewatupia virago mabeki wawili wa Kiganda na mshambuliaji mmoja Msudani.

Lakini ikamsajili Mganda mwingine Joseph Owino aliyewahi kuichezea kabla ya kuondoka baada ya kuumia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic