COASTAL UNION |
Pamoja na ushindi mnono wa Simba na sare ya Yanga dhidi ya Prisons, Ligi Kuu Bara imeendelea kuonekana ni ngumu.
DAR-CHAMAZI:
Azam FC ikiwa nyumba Chamazi Complex imbanwa na sare ya bao 1-1 na Ashanti United iliyopata pointi moja muhimu zaidi. Kipre ndiye aliifungia Azam FC na Mtangalu akaisawazishia Ashanti.
BUKOBA:
Lakini Kagera Sugar ikapaa kwa kuifunga JKT Oljoro kwa mabao 2-1, Godfrey alianza kuifungia Kagera, Shaibu Nayopa akaisawazishia Oljoro kabla ya bao la ushindi katika dakika ya 90 lililofungwa Maregesi Mangwa.
TANGA: Coastal Union wakiwa nyumbani, walilazimika kusubiri mkwaju wa penalti wa Jerry Santo kupata sare ya 1-1 dhidi ya Rhino.
PWANI:
Ndugu walikuwa wanakutana kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mabatini na Ruvu Shooting wakaibuka na ushindi wa bao 1-0.
MANUNGU-TURIANI
Kigogo mwingine Mtibwa Sugar naye akabanwa kwa suluhu dhidi ya Mbeya City kwenye dimba lake la nyumbani la Manungu.
0 COMMENTS:
Post a Comment