Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union,
Nassor Binslum, amecharuka na kuhoji kuhusiana na mwamuzi Martin Saanya.
Saanya alishindwa kuchezesha vizuri
katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Costal Union ambayo matokeo yake
yalimalizika kwa sare ya mabao 1-1.
Kupitia kwenye ukuta wake wa Facebook,
Binslum ameandika haya yafuatayo…
Martin Sanya anafungiwa mwaka
mzima kwa kosa la kuipa Coastal union penalty ya dk 95 au kwa kuboronga ktk
maamuzi yake mengi, na kwanini afungiwe mwaka mzima wakati TFF hawa hawa ndio
waliokuwa wakimpangia kila mechi ya coastal na yanga mkwakwani tangia coastal
irejee ligi kuu refa ni martin sanya, na matokeo ya mechi mbili zote hizo
mkwakwani coastal ilipoteza 1-0 na 2-0 refa akiwa sanya, kipindi coastal
inapoteza zile mechi tena refa ni huyohuyo sanya hatukusikia wachambuzi wala
TFF kumtoa kasoro sanya lkn leo baada ya refa huyohuyo wa TFF kwa mechi za
Coastal na Yanga matokeo kuwa magumu kwa Yanga hususan kuipa coastal penalty ya
mwishoni kabisa mwa mchezo Martin Sanya amekua haoni vizuri, hajui sheria na
makosa mengi kumtwisha na kibaya zaidi adhabu aliyopewa ni dhahiri imeonesha
kuna watu walichukizwa na yale matokeo mpaka kupelekea kumpa adhabu ya kumkomoa
ya mwaka mzima...........sote tunakubali maamuzi mengi ktk mechi ile yalikua na
utata lkn TFF hawahawa wanasahau ni sanya huyuhuyu aliyewapa mbeleko Simba
mechi ya ngao ya hisani na Azam kwa kuwanyima Azam Fc penalty mbili za wazi na
pia kuruhusu goli la okwi akiunawa mpira lkn hatukuona adhabu hata ya kumfungia
mechi moja asichezeshe, kwanini waamuzi wafungiwe kwa kukosea maamuzi ya mechi
za MAPACHA ila timu ndogo na za mikoani zinapoonewa na maamuzi mabovu
isichukuliwe sheria kali kama wanayomtoa muhanga leo MARTIN
SANYA...!!!!!!?????????
Bin slum kwani ni MGENI hapa nchini? :-d
ReplyDelete