Uongozi wa klabu ya Coastal Union umezidi kuutia
presha ule wa mabingwa Tanzania Bara, Yanga kutokana na ukimya wao.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Mohammed Bin
Slum ambaye pia ni mdhamini wa klabu hiyo amesema anashangazwa na uongozi wa
Yanga kuendelea kukaa kimya.
“Kilichotokea hakikuwa kitu cha kiungwana, hivyo
tulitegemea kuona uongozi wa Yanga unazungumza jambo kwa lengo la kukemea.
“Kuendelea kukaa kimya ni sawa na kuonyesha hawajali
na ninashangazwa na hili,” alisema.
Mashabiki wa Yanga walilishambulia basi la Coastal
Union wakati likitoka uwanjani baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara ambayo
ilimalizika kwa sare ya mabo 1-1.
Coastal Union walisawazisha katika dakika ya 90 kupitia
mkwaju wa penalti wa nahodha Jerry Santo, hali iliyowakasirisha mashabiki hao wa
Yanga.
Mchezaji mmoja wa Coastal Union alijeruhiwa mara
baada ya basi hilo kushambuliwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment