Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake nchini
Ethiopia umethibitisha kukamatwa kwa mshambuliaji wa zamani wa Simba Joseph
Kaniki akiwa na madawa ya kuleya.
Pamoja na Kaniki, bondia Mkwanda Matumla naye
amekamatwa wakiwa pamoja kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini
Addis Ababa, Ethiopia.
Blog hii ilikuwa ya kwanza kuandika jana kuhusiana
na kukamatwa kwa wawili hao lakini ikawa kazi kubwa kupata uthibitisho kutokana
na ofisi nyingi za serikali kuwa zimefungwa Jumapili.
Lakini Kaimu balozi wa Tanzania nchini Ethiopia,
Samuel Shelukindo amethibitisha hilo.
Amesema wamepewa taarifa hizo na wamezungumza nao na
wakasema hawakuwa wakijua kuhusiana na mizigo hiyo.
“Kaniki amesema mzigo huo alipewa pale Mombasa na
aliyempa anajuana vizuri na Mkwanda kwa hiyo alikuwa kama amebeba tu.
“Ukweli tulichofanya ni kuacha sheria ichukue mkondo
yake, lazima wajibu kesi iliyo mbele yao,” alisema Shelukindo.
Kaniki amekuwa akiishi nchini Sweden kama ilivyo kwa
Mkwanda ambaye ana mtoto mmoja na mwanamke wa Kiswidi.
Mwaka juzi Kaniki alisajiliwa na klabu ya daraja la pili ya Sweden ya Konyar Spor lakini hata hivyo hakudumu.
0 COMMENTS:
Post a Comment