Kocha Mkuu wa Simba ameanza kutengeza safu imara ya ushambuliaji
ambayo itakuwa pacha.
Abdallah Kibadeni amesema anataka kuwaunganisha washambuliaji wake
wawili, Mtanzania, Betram Mombeki na Mrundi, Amis Tambwe.
Kibadeni amesema ameridhishwa na viwango vyao lakini sasa ni aina
ya uchezaji ambayo anaifanyia kazi.
“Wanacheza katika kiwnago kizuri, lakini sasa ni kuwatengeneza ili
wacheze kama wachezaji pacha.
“Ni suala linalohitaji muda, nimeishaanza hiyo kazi na huenda
matunda yataanza kuonekana ingawa ni hatua kwa hatua,” alisema.
Mombeki anaonekana ni mzuri katika ufungaji hasa anapokuwa karibu
na lango lakini Tambwe ana kasi na mjanja.
Kingine kizuri kwa Mombeki ni umbo lake na anajua kulitua vizuri
wakati Tambwe ana uwezo wa kupicha chenga na mwepesi kuachia mashuti ya
kushtukiza.
Iwapo Kibadeni atafanikiwa kuwaunganisha, huenda Simba ikawa na
safu kali zaidi ya ushambuliaji msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment