Benchi la ufundi la Prisons ya Mbeya bado lina matumaini ya
kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara.
Prisons ndiyo inaburuza mkia katika msimamo wa ligi hiyo baada ya
kucheza mechi mbili.
Kocha Mkuu wa Prisons, Jumanne Chale amesema ligi bado ni mbichi.
Akizungumza na Championi
Jumatatu, kocha huyo alisema kutofanya kwao vizuri mwanzoni mwa ligi siyo
kwamba timu yao imeshindwa kabisa, bali bado wanaisoma ligi.
“Timu yetu ya Prisons imepoteza michezo miwili mfululizo, siyo
kwamba ndiyo tumepoteza mwelekeo, ni mapema sana, zaidi tunafanya marekebisho
kwa ule upungufu tulioubaini.
“Wapinzani wetu mechi ijayo wajipange, japo ni timu kubwa na
inafanya vizuri.
“Ni mapema sana japo tumefanya vibaya lakini tunazidi kufanya
maandalizi ili tuweze kufanya vyema katika mechi zijazo na kuwa katika nafasi
nzuri, tofauti na sasa tupo nafasi ya mwisho,” alisema Chale.
Prisons ilianza ligi kwa kufungwa 3-0 na Ruvu Shooting, baadaye
ikafungwa kwa idadi kama hiyo dhidi ya JKT Ruvu.
0 COMMENTS:
Post a Comment