September 9, 2013


Mshambuliaji mkongwe wa Cameroon, Samuel Eto'o ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya nchini Indomitable Lions.
Taarifa zimeeleza kwamba Eto’o ameamua kustaafu kutokana na masuala ya kifamilia lakini kumekuwa na taarifa kwamba haelewani na kocha Mjerumani, Volker Finke.

Eto’o ,32, ambaye hivi karibuni amejiunga na Chelsea chini ya Jose Mourinho ameamua kustaafu na taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimeeleza alipendekeza kuteuliwa kwa kipa Carlos Kameni na mshambuliaji Achille Webo lakini kocha huyo alikataa na tafrani kati yao likaanza.

Hivi karibuni, Eto’o aliichezea Cameroon mechi muhimu ikiwa ni siku chache baada ya kurudishwa timu ya taifa na kona aliyopiga ikazaa bao muhimu lililofungwa na Aurelien Chedjou.

Bao hilo liisaidia Cameroon kuvuka hatua ya mwisho kuwania kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil na ratiba itapangwa Septemba 16 jijini Cairo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic