Siku chache baada ya wazee kumfukuza,
uongozi wa Yanga leo umewatambulisha viongozi wapya watatu wa klabu hiyo,
akiwemo Mkenya Patrick Naggi.
Naggi alitimuliwa na wazee wa Yanga
ambao walikuwa na mambo kadhaa ya kuhoji likiwemo lile la uanachana.
Lakini leo, uongozi wa Yanga, umesema
Naggi na wenzake watakuwa katika klabu hiyo wakifanya kazi kadhaa hadi hapo
zitakapotangazwa nafasi zipi watashika.
Utambulisho huo wa leo umeafanywa na
Makamu Mwenyeki wa Yanga, Clement Sanga ambapo mbali na Naggi, pia
aliwatambulisha George Magani mwenye utaalamu wa biashara pamoja na Benno
Njovu, ambao wote wanaingia katika sekretarieti ya klabu hiyo, ambapo baada ya
miezi miwili ijayo watapangiwa kazi mpya ya kufanya katika uongozi wa klabu hiyo.
Sanga alisema tayari wote ni wanachama wa
Yanga lakini hawajakabidhiwa kadi zao tu.
Wazee wa Yanga walimtaka Naggi kuondoka
klabuni hapo kwa madai hakuwa mtu aliyefika hapo kwa kufuata taratibu.
Katika mkutano wa waandishi leo, Naggi
na wenzake hawakutakiwa kuzungumza lolote.
0 COMMENTS:
Post a Comment