Hatimaye mama wa mshambuliaji wa zamani wa
Simba, Khalfan Ngassa amepumzishwa baada ya kuzikwa jana mjini Mwanza.
Bibi huyo ambaye ni bibi wa mshambuliaji
wa Yanga, Mrisho Ngassa alizikwa jana katika makaburi ya Kirumba jijini humo.
Ngassa amesema kila kitu kimekwenda
vizuri na wamefanikiwa kufanya kila kitu kiende vizuri.
“Tunamshukuru Mungu, tumempumzisha bibi
na ndugu, majirani na jamaa tumeshirikiana nao vizuri hadi mwisho. Tunatoa shukurani
nyingi sana kwao,” alisema Ngassa ambaye alikuwa Mwanza.
Bibi huyo alifariki siku tatu zilizopita
jijini humo baada ya kuugua kw amuda mfupi.
0 COMMENTS:
Post a Comment