KAPOMBE AKIWA MAZOEZINI NA AS CANNES, HII ILIKUWA KABLA YA KUFANYIWA UPASUAJI WA KIDOLE (PICHA NA KEVIN MESA, CANNES, UFARANSA) |
Na Saleh Ally
Kitengo cha afya cha klabu ya AS Cannes kimemtaka mchezaji wake mpya kutulia ndani muda mwingi na kuepusha kutembea bila ya sababu za msingi.
Uamuzi huo
unatokana na kutaka kuona Kapombe anapoba haraka na kurejea dimbani kwa ajili
ya kuichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa.
Jean Pierre
ambaye ni mmoja wa wahusika katika kitengo cha tiba cha timu hiyo amesema jana
kwamba Kapombe anaendelea vizuri.
“Matumaini yetu ni apone haraka na kurudi
uwanjani. Tumempa siku kumi na tano za kupumzika kutokana na tatizo hilo la
kidole.
“Lakini
lazima apumzike, tumemtaka ahakikishe asitembee bila ya kuwa na sababu za
msingi. Aupumzishe mguu kwa muda mwingi ili imsaidie kupona haraka,” alisema
Pierre.
“Tuna
wachezaji wengine watatu katika kikosi chetu ni wagonjwa pia, tumekuwa na
utaratibu wa kuwafuatilia kwa ukaribu kabisa na kama Kapombe atapona haraka,
ataanza mazoezi ya taratibu kabla ya kujiunga na wenzake mazoezini,” alisema.
Wiki
iliyopita, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen alitangaza Kapombe hatajiunga
na kikosi chake pamoja na kuwa amemuita na hali hiyo inatokana na kufanyia
upasuaji wa kidole cha mguu.
Kapombe aliyefanikiwa
kupata nafasi hiyo kwa juhudi za Denis Kadito, wakala wa kuuza wachezaji, amejiunga
na timu hiyo akitokea Simba ambayo aliichezea kwa mafanikio kabla ya kutajwa
mchezaji bora wa msimu uliopita na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
(Taswa).
0 COMMENTS:
Post a Comment