September 2, 2013

TORRINGTON (KULIA) AKIFURAHI MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA KUONYESHA MOJA KWA MOJA MECHI ZA LIGI KUU, KULIA KWAKE NI MAKAMU WA RAIS WA TFF, ATHUMAN NYAMLANI, NAYE 'AKIANGUKA'

Uongozi wa runinga ya Azam Tv umesema unatarajia kutengeneza mamilioni ya fedha kupitia Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini ukakataa kuelezea kwa undani zaidi.

Akijibu maswali ya waandishi hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Tv, Rhys Torrington alisema matarajio yao ni kuingiza mamilioni ya fedha, lakini hawawezi kuweka hadharani mipango yao ya biashara.

“Kweli tunatarajia kuingiza mamilioni ya fedha kupitia ligi kuu, hii ni sehemu ya mikakati ya kutengeneza fedha lakini hatuwezi kuanika mipango yetu.

Hata hivyo, Torrington aliwataka Watanzania kujivunia Azam Tv kwa kuwa ni chombo kinachimilikiwa na Mtanzania.
“Ushauri wangu ni kwenu kujivunia Azam Tv kwa kuwa ni ya Mtanzania na sasa itaonyesha mechi za ligi kuu. 

Tutaanza majaribio hivi karibuni na siwezi kuruhusu matangazo yaende hewani bila ya kuwa na kiwango bora ninachotaka,” alisema.

Azam Tv inatarajia kuanza majaribio yake wiki hii na kama bosi huyo atakuwa ameridhika na kiwango itaanza kurusha matangazo yake.

Azam Tv imeingia mkataba miaka mitatu wa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na bodi ya ligi ambao thamani yake ni Sh bilioni 5.6 na kila klabu itakuwa ikipata Sh milioni 100 kila msimu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic