KOCHA YANGA, ERNIE BRANDTS |
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa siku 14 kwa klabu za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza (FDL) kuwasilisha
mikataba ya makocha wao.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF iliyokutana Septemba
12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha mikataba ya mabenchi yao ya
ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni. Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia
Septemba 17 mwaka huu.
Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba hiyo na
vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment