December 27, 2013


Kiungo mpya wa Yanga, Said Dilunga alijikuta akishindwa kuhimili kuivaa jezi namba 25 ya beki wa pembeni wa Simba, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe uliozikutanisha timu hizo na kujikuta akiitoa na kuvaa fulana ya mazoezi.

KIIZA AKIMPA NENO DILUNGA KUHUSIANA NA JEZI NAMBA 25

Tukio hilo lilitokea mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ulioisha kwa Simba kushinda mabao 3-1 ambapo kiungo huyo alibadilishana jezi ya juu na beki huyo mwenye umbo dogo na kasi awapo uwanjani.
DILUNGA ANAONEKANA KUELEWA SOMO HUKU KIIZA AKIWA SIRIAZ KINOMA KAMA AFANDE

SOMO LIMEELEWEKA, ANAIVUA JEZI HIYO YA ZAMANI YA OKWI

SALEHJEMBE ililishuhudia tukio hilo mwanzo mwisho lilimuona kiungo huyo baada ya kubadilishana akaitwa na mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza na kunong’onezana kitu, walipomaliza Dilunga akaitoa jezi hiyo iliyokuwa ikivaliwa na Emmanuel Okwi kipindi yupo Simba ambaye kwa sasa yupo Yanga kisha akaichukua ya Yanga na kuivaa.

Alipotafutwa Dilunga ili kujua sababu za kuitoa jezi hiyo huku wachezaji wenzake wa Yanga wakiwa na uzi wa watani zao hao alisema “Jezi ile niliamua tu kuitoa na kuvaa ya mazoezi lakini niliondoka nayo na nipo nayo hapa nyumbani. Baba Ubaya ni rafiki yangu na nimewahi kucheza naye kipindi cha nyuma.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic