October 15, 2021

 


HAJI Manara aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Simba na sasa ni Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa ameandaa mawakiki 10 wa kusimamia kesi yake na Simba.

Manara amebainisha kuwa yupo kwenye mpango wa kuishtaki klabu hiyo kwa madai ya kumfanyia dhuluma na akitaka kulipwa stahiki zake kwa muda wa miaka 6.

Ofisa huyo ambaye yupo kwenye kipengele cha kuwania tuzo kwa muhamasishaji bora kwa msimu wa 2020/21 ambao alikuwa Simba amesema kuwa hatakubali kuona jasho lake linapotea.

"Nitaenda mahakamani kudai haki yangu, nawadai Simba pesa nyingi wamenitumia miaka zaidi ya sita.

"Nimefanyiwa dhuluma, hawa sio binadamu kwa kweli mimi nina kifua sijawahi kusema ila siku nikisema mtanielewa, kisa umaarufu eti mimi ananichukia.

"Na iliwauma zaidi mimi kwenda Yanga,walinifanyia mambo mengi mabaya na nitadai haki yangu nimeandaa mawakili 10," alisema Manara.

6 COMMENTS:

  1. Kesi hii itakuwa dhidi ya Haji Manara aliekuwa amelewa wakati akiwa simba na Haji Manara wa Yanga aliechanganykiwa,kazi ipo😷
    Kesi ya madai ya ukweli hata wewe mwenyewe binafsi unajiwakilisha na unatoboa.Yeye Manara hata aweke mawakili elfu moja alishaharibu tayari na ndio maana anatapatapa kama samaki alieangukia mchangani. Manara hana kesi labda dhamira yake kubwa na hao wanaomtumia ni kuwatoa Simba mchezoni kwenye hii wiki yao ya ligi ya mabingwa.

    ReplyDelete
  2. Duu huyo Haji Manala amejua juzi Kama alionewa,kumbe Haji sio mtu Makini mpaka akafanya kazi miaka mingi Bila makubaliano.kesi rahisi kwa simba

    ReplyDelete
  3. Huyu hana analowaza zaidi ya kutapatapa. Yeye pamoja na wajinga wenzake wanaomtumia ndio wamekaa wakabuni kuanzisha hilo zogo eti kuivuruga simba ili ifungwe, wamenoa. Mbinu za kitoto wahangaike na litimu lao. Acha aende hata mahakama ya dunia poa tuu

    ReplyDelete
  4. Dhuluma gani wakati hakukuwepo mkataba! :>) . Kwa ufupi, Simba haijawahi kuwa na mfanyakazi anayeitwa Haji sunday Manara, kwa hiyo hakuna madai yoyote kutoka kwa mtu huyo :>)

    ReplyDelete
  5. Anayemchimbia shimo nduguye hutumbukia mwenyewe na ngoma ikilia sana itarajiwe kupasuka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic