September 12, 2019


Na George Mganga

Mchezaji wa zamani Yanga, Edibily Lunyamila, amemshangaa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, kusema anahitaji straika ili kuboresha safu yake ya ushambuliaji.

Lunyamila amefuguka hayo kutokana na kauli aliyoitoa Mbegiji huyo juzi, kuwa safu yake bado ina mapungufu na inapaswa usajili wa straika mwingine ufanyike.

Aussems alieleza kuwa uwepo wa Kagere peke yake haiwezi kuleta makali ndani ya safu hiyo wakati huohuo Nahodha John Bocco akiwa hajawa fiti baada ya kutoka mazoezi mepesi hivi karibuni akitoka kuwa majeruhi.

Lunyamila amesema Aussems hana sababu ya kulalamika kwani ligi ndiyo kwanza imeanza na ni mapema kuanza kulalamika.

Alieleza kuwa wakati dirisha la usajili linafunguliwa alikuwa ana nafasi ya kusajili kama aliona mapungufu huku akimshauri hivi sasa anapaswa kutumia wachezaji mbadala kwani kikosi chake ni kipana.

"Aussems hana haja ya kulalamika hivi sasa sababu ligi ndiyo kwanza imeshaanza.
"Nadhani anapaswa kufanya kutumia wachezaji mbadala badala ya kumtegemea Kagere na Bocco sababu ana kikosi kipana.

"Kama unataka unalalamika Bocco kuumia, siku Kagere akiumia atasemaje?

"Ni vema akatuliza kichwa kipindi hiki ajaribu kuwatumia viajana wengine ambao wapo pale Simba, naamini wanaweza kumuonesha kile anachokitaka kuliko kutaka usajili mwingine ufanyike mapema hii wakati timu imecheza mechi moja pekee."


11 COMMENTS:

  1. Huyo hana la kusema na anataka kuandika tu. Kwanini hamlaumu Zahera Kwa malalamiko yake yasiyokwisha na yasiyo ya faida

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ile tabia yako ya kupiga puli asubuhi,umeona sasa unapumbika!

      Delete
  2. Anonymous acha lugha chafu, huu ni mpira. Fair play, fair language.

    ReplyDelete
  3. Lunyamila punguza hilo tumbo kwanza utafikiri vizuri

    ReplyDelete
  4. Huenda ansjihisi kuwa anaujuzi zaidi WA kumpita Aussems

    ReplyDelete
  5. Hivi kocha wa simba amelalamika au aliulizwa swali ndiyo akajibu kuhusu matatizo ya straiker wake? Mana watu wameshachukulia km topic hivi

    ReplyDelete
  6. Enter your comment...Yani Mwandishi Huweki Habali Inayo Eleweka Habali Nyingi Hapa Ni Za Uongotu

    ReplyDelete
  7. Toka lini Chui akamshauri swala jinsi ya kukimbia? Lunyamila ni Yanga lialia, haitotokea siku akaipa ushauri mzuri Simba. Ni bora aongeze nguvu namna ya kukusanya michango.

    ReplyDelete
  8. Hivi ushabiki wa Tanzania,ni sawa na ukabila au udini,usio na maana,Lunuamila kweli yeye ni mchezaji wa Yanga wa zamani,kutoa maoni Kama mtanzania baada ya tamko la kocha,halina ubishi wa kumtolea maneno yasiyo faa,ukiangalia kikosi Cha Simba chote ni kizuri na Kila mchezaji Ana mbadala wake,hili halina ubishi,Sasa kocha anataka wachezaji wa Sina gani,atumie hao hao alionao wanaweza kuchukuwa ibingwa hata bila bocco au kagere akiwatumia vizuri .tuache ushabiki wa kitoto,tuwe wa kweli bila kaungalia aliye sema ni nani.maoni ni maoni Kila atakaye sema kukosoa ilimladi hajaipamba timu yako basi hiyo Yanga au Simba hatutoendelea tutaishia matusi tu na so ustaarabu


    ReplyDelete
  9. Mgonjwa huyu badala ya kusema Zahera kila siku analialia anasema Aussem.
    Angalia chama lako au timu unayofundisha.simba another level.nini kinakuwasha

    ReplyDelete
  10. Tatizo la WaTz wengi wanaandika bila kumfikiria.
    Sasa kwa kikosi cha Simba kuna haha gani ya kulalamika hakuna straika Wakati kikosi ni kipana.
    Tuache ushabiki was kishamba, angalieni uhalisia.
    Kwa Sasa hakuna sababu ya kocha kulalamika,l Kama uwezo wake umeishia hapo, hawezi kutumia wachezaji mbadala.
    Kwa wanaofuatilia soka, mtakumbuka kuna mchezaji Kama Said Mwamba Kizota alikua namba 9 hatari, lkn kocha akamrudisha beki na akafanya vzr Sana.
    Kwakifupi kocha anatakiwa kuwa mbunifu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic