Wazee wa Yanga wamesema hawana tatizo na
uongozi wao kumrudisha Patrick Naggi.
Kiongozi wa wazee hao, Ibrahim Akilimali
amesema kama utaratibu umefuatwa wao hawana tatizo.
“Unajua msifanye ionekane kama tulikuwa
na malumbano na uongozi wetu. Kikubwa tulipinga utaratibu kutofuatwa.
“Lakini kama kila kitu kitafuata
utaratibu, basi sisi tuko tayari kumpokea mtu yoyote ambaye anakuja kufanya
kazi kwa ajili ya maendeleo ya klabu yetu,” alisema Akilimali.
“Hivyo tunamkaribisha na utaratibu
umefuatwa ndiyo tulichokuwa tunataka.”
Hivi karibuni, Akilimali aliwaongoza wazee hao kumtimua Naggi ambaye alitinga klabuni hapo 'kinyemela'.
Utambulisho wa leo umeafanywa na Makamu
Mwenyeki wa Yanga, Clement Sanga ambapo mbali na Naggi, pia aliwatambulisha
George Magani mwenye utaalamu wa biashara pamoja na Benno Njovu, ambao wote
wanaingia katika sekretarieti ya klabu hiyo, ambapo baada ya miezi miwili ijayo
watapangiwa kazi mpya ya kufanya katika uongozi wa klabu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment