Uongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA), umeihakikishia usalama Yanga pamoja na mashabiki wake kesho kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Kesho Yanga inashuka dimbani tena Sokoine, safari hii kuivaa Prisons ya hapo Mbeya.
Mwenyekiti wa chama hicho, Elias Mwanjala amesema Yanga hawana sababu ya kuwa na hofu kwa kuwa kila kitu kitaenda vziur.
“Tumefanya kikao kuhusiana na ulinzi utakavyokuwa na mambo yamekwenda vizuri. Tunaweza kuwahakikishia Yanga usalama na tunaomba mambo yaende vizuri.
DEREVA WA YANGA AKITIBIWA |
“Kikuba ni kuwasisitiza wao pia kuwa watulivu na mambo yaende vizuri, unajua hatupendi vurugu hapa Mbeya na wala si kawaida yetu.
“Inawezekana vijana wanaona kawaida tu lakini mambo yanaweza kuwa tofauti kabisa,” alisema Mwanjala.
Kabla ya mechi hiyo, Jumamosi iliyopita mashambiki waMbeya City waliishambulia na kusababisha maumivu makali kwa dereva wa gari la Yanga
Lakini walivunja vioo vya magari kadhaa likiwemo basi la Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment