September 17, 2013





Mshambuliaji nyota wa Galatasaray, Didier Drogba amesema wana uhakika wa kushinda katika mechi yao dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Ali Sami Yen jijini Istambul, Uturuki.

Drogba raia wa Ivory Coast amesema msimu uliopita katika ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Madrid waliwatoa kwa jumla ya mabao 3-2.


“Hata sisi tuna uwezo wa kufanya hivyo kwa kuwa timu yetu ni nzuri na ina wachezaji wenye uwezo.

“Kikubwa ni sisi kujituma na kuhakikisha tunacheza kwa asilimia mia na kuibuka na ushindi,” alisema Drogba (32).

Kwa upande wa uongozi wa klabu hiyo maarufu zaidi nchini Uturuki, umeeleza kiungo wake nyota Wesley Sneijder yuko fiti kuwavaa Madrid leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic