Azam FC ya Tanzania ambayo ilishika nafasi ya pili msimu uliopita
itaanza michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kucheza na Ferroviário da Beira ya
Msumbiji.
Kama itafanikiwa kuvuka dhidi ya Wamakonde hao wa Msumbiji, basi Azam
FC inayonolewa na kocha kutoka Cameroon itakutana na Zesco ya Zambia.
Kwa upande wa Zanzibar, wawakilishi wa kisiwa hicho katika michuano ya
Shirikisho ni Chuoni na wamepangwa kuanzia ugenini dhidi ya How Mine ya
Zimbabwe.
Kombe la Shirikisho
Azam Vs Ferroviário da Beira
Februari 7-9, marudio Februari 14-16
How Mine Vs Chuoni
Februari 7-9, marudio Februari 14-16







0 COMMENTS:
Post a Comment