May 16, 2018


Na George Mganga

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amekemea tabia ya baadhi ya Waandishi wa Habari kuwahoji watu ambao wamekuwa wakipinga mabadiliko.

Manara ameyaeleza hayo leo alipoitisha kikao na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Serena Hotel, jijini Dar es Salaam akisema ni suala ambalo halipaswi kuendelezwa.

Ofisa huyo wa Habari ndani ya Simba, ameeleza kutofurahishwa na tabia hiyo ambayo imekithiri kwa baadhi ya Waandishi kufanya mahojiano na watu wa aina hiyo ambao wamekuwa kazi yao ni kupinga tu bila kujua faida ya mwelekeo wa soka la Tanzania.

Manara amesema inabidi sasa baadhi ya vyombo vya habari viache tabia hiyo kwani imekuwa ikidhorotesha maendeleo ya klabu za Tanzania na mwisho wa siku kuzidi kusalia nyuma badala ya kusonga mbele.

Kitendo hicho cha wapinga mabadiliko kuzidi kufanyiwa mahojiano na watu wasiokubali kwenda na wakati kimezidi kuharibu ramani na taswira ya soka la Tanzania, kwani watu hao ambao wamekuwa wakipinga pale klabu zinapotaka kuendelea kutoka hatua moja kwenda nyingine wamekuwa hawana nia nzuri na mpira wa nchi hii.

Manara ameyaeleza hayo kutokana na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakihojiwa na kueleza kuwa klabu ni za kwao na kusahau kuwa zipo chini ya wanachama huku wakipinga mfumo wa kisasa ambao Simba wanataka kuwa wa kwanza kuuanzisha hapa Tanzania.

Simba inaenda kufanya mkutano mkuu na wanachama wake Jumapili ya wiki hii utakaoenda kuweka historia ya soka la Tanzania na pengine Afrika Mashariki na Kati kwa kufanya mabadiliko ya kikatiba ili kuingia rasmi kwenye mfumo wa kisasa kiuendeshwaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic