Simba leo itacheza na TP Mazembe mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali utakaopigwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00.
"Mechi itakuwa ngumu na ya ushindani ila tupo tayari kupambana na tutaingia kwa mtindo wa kushambulia ili kupata mabao kwa kuwa tupo nyumbani hatuna mashaka.
"Tupo tayari kushinda, tumefanya kila kitu ili tushinde, itakuwa mechi ngumu lakini nina uhakika kwa ushirikiano ambao tutapata kutoka kwa mashabiki wetu na namna wachezaji watajituma tunaweza kuwa na jambo zuri” amesema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment